Gaza: Wanawake na watoto zaidi ya Elfu Moja kupokea matibabu barani Ulaya
Wanawake na watoto karibia Elfu Moja wanaohitaji huduma za kimatibabu wanatarajiwa kuondolewa katika Ukanda wa Gaza na kupelekwa barani Ulaya kutibiwa, kwa mujibu wa WHO barani Ulaya.
Imechapishwa:
Taarifa ya Hans Kluge, afisa kutoka shirika la WHO bara Ulaya, inasema mpango huo utaoongozwa na WHO pamoja na mataifa mengine ya EU yanayohusika kwenye shuguli hiyo.
Siku ya Alhamis, wataalam wa uchunguzi kutoka Umoja wa Mataifa katika ripoti yao, walithibitisha kwamba Israeli inalenga kimakusudi vituo vya afya katika Ukanda wa Gaza.
Ripoti hiyo aidha ilieleza kwamba wanajeshi wa Israeli kando na kushambulia vituo vya afya pia inawatesa wahudumu wa afya na kuwaua wengine.
Vilevile ripoti hiyo ya UN pia iliituhumu Israeli kwa kutekeleza makosa ya uhalifu wa kibinadamu.
Rik Peeperkorn, mwakilishi wa WHO katika maeneo yanayokaliwa na raia wa Palestine, mwezi Mei alieleza kwamba karibia watu Elfu 10 walikuwa wanahitaji kuondolewa kwa dharura katika Ukanda wa Gaza kwa ajili ya matibabu.
Shirika la WHO ukanda wa bara Ulaya tayari limewasaidia watu 600 wanaohitaji matibabu kuondoka katika Ukanda wa Gaza na kuwapeleka katika mataifa saba ya EU tangu kuzuka kwa mapigano mwezi Oktoba mwaka wa 2023.