Shinji Mikami
Mandhari
Shinji Mikami (alizaliwa Agosti 11 1965) ni Mjapani mkurugenzi wa michezo ya video za kompyuta, ni mkurugenzi na mtayarishaji wa video hizo.
Alianza kazi yake huko Capcom mwaka wa 1990, aliendelea kuongoza makampuni hayo yanayotengeneza na kusambaza michezo hiyo mpaka 2006.
Mikami alizaliwa katika kisiwa cha Yamaguchi na kukulia katika kisiwa cha Honshū, Kama kijana mwenye nguvu, Mikami alikuwa dereva wa mashindano ya Formula one. Pia alikuwa anajishughulisha na kuigiza filamu.
Akiwa kijana alififunza karate na taekwondo, alisomea mambo ya bidhaa chuo kikuu, Mikami alihitimu katika Chuo Kikuu cha Doshisha, ambapo alijitokeza katika utafiti wa bidhaa mbalimbali.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shinji Mikami kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |