Kusimamishwa kwa msaada wa Marekani kumeathiri operesheni za kibinadamu DRC
Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Bruno Lemarquis, leo (11 Feb) ameeleza kwamba uamuzi wa serikali ya Marekani kusimamisha msaada wa kigeni “ni chanzo kikubwa cha wasiwasi,” kwani mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa na mengine yasiyo ya kimataifa yanayofanya kazi mashinani yameathirika vibaya, kama sio kusitisha kabisa shughuli zao.