Sally McLellan
Sally McLellan (aliyezaliwa 19 Septemba 1986 huko Sydney, Australia) ni mwanamichezo wa Australia ambaye ni mtaalamu katika mita 100 na mita 100 ya kuruka viunzi. McLellan ndiye anashikilia rekodi ya Australia kwa mita 100 ya kuruka vikwazo na yeye ndiye mwanariadha kasi wa pili wa Australia nzima katika mbio ya 100m. Wakati wa Olimpiki ya 2008, yeye alishinda medali ya fedha katika mbio ya 100m ya vikwazo kwa muda wa sekunde 12.64.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Sally alizaliwa mjini Sydney na wakahamia Gold Coast alipokuwa umri wa miaka 8. Ilikuwa pale, wakati yeye bado alikuwa katika shule ya msingi,ndipo kipaji chake cha riadha ikaonekana na Sharon Hannan ,ambaye ni kocha wake hadi sasa. [10] Sally alipata umaarufu katika mwaka wa 2001,akiwa umri wa miaka 14 tu,akashinda mbio ya 100m ya Australia ya walio chini ya umri wa miaka 20. Baada ya shida za kujeruhiwa katika mwaka wa 2002,alikimbia mbio yake ya kimataifa ya kwanza katika Mbio ya Dunia ya Ubingwa ya Vijana,Sherbrooke,Kanada na akashinda mbio ya 100m kuruka viunzi. Mwezi uliofuata,akiwa umri wa miaka 16 ,aliwakilisha Australia katika ngazi ya Mashindano ya Mabingwa ya Dunia ya 2003,Paris,Ufaransa kama mmola wa wanariadha wa timu ya mbio ya 4x100m. Ilipofika mwaka wa 2004,alishinda medali ya shaba katika mbio ya 100m katika Mbio ya Dunia ya Vijana ya Mabingwa, na akakosa tu kwa kidogo sana medali katika mbio ya 100m ya kuruka viunzi.
Katika Michezo ya Madola ya 2006,Melbourne,Australia,Sally alitegwa na kiunzi na akaanguka katika fainali ya mbio ya 100m ya kuruka viunzi, hii ikamfanya akose medali. Mnamo mwaka wa 2007, yeye aliendelea kushindana katika mbio zote mbili,100m na 100m ya kuruka viunzi, akifika semifainali katika zote mbili katika Mashindano ya Mabingwa ya Dunia ,Osaka,Ujapani. Hata hivyo katika Olimpiki ya 2008,alibadilisha lengo lake na akaamua kufanya bidii katika mbio ya 100m ya kuruka viunzi pekee yake. Uamuzi huo ulikuwa bora na Sally akashinda medali ya fedha katika fainali kubwa ambapo aliyedhaniwa kushinda ,Lolo Jones aliteguka na akaanguka.Mbio hiyo ilihitaji usaidizi wa picha ili kuchagua washindi wa fedha na shaba. Baada ya kutangazwa kwa matokeo rasmi, McLellan alisherehekea sana kwa furaha akiwa mshindi wa medali ya shaba,Priscilla Lopes-Schliep.Mahojiano ya hapo baasaye yalionyesha kuwa alikuwa na furaha na hisia nzuri nyingi ya mbio hiyo.
McLellan alikuwa katika fomu nzuri katika msimu wa Uropa wa 2009,huku akishinda mbio tano kati ya saba na kuvunja rekodi ya Australia na Oceania ya mbio ya 100m ya urukaji viunzi katika mbio za Herculis hapo Julai,akiwa na muda wa sekunde 12.50.Muda huu ulikuwa kasi kwa sekunde 0.03 kuliko ule aliokuwa ameweka mwaka uliokuwa umepita.. Hata hivyo, aliathiriwa na maumivu mgongoni katika matayarisho ya Mbio ya Mabingwa ya Dunia ya Berlin,Ujerumani na kamaliza akiwa #5 katika fainali ya 100m ya kuruka viunzi. [12]
Maisha ya Kibinafsi.
[hariri | hariri chanzo]Sally alilelewa na mama pekee yake,aliyefanya kazi mbili ili kupata pesa ya kutosha ya kumsaidia kazi ya bintiye. Mwishoni mwa mwaka wa 2008, aliweka ahadi ya ndoa na Kieran Pearson, hawa wakiwa wamekuwa pamoja tangu mwaka wao wa mwisho wa Shule ya Upili ya Helensvale State,Gold Coast. [14]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Katika Mashindano Mbalimbali
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Mashindano | Eneo la Mashindano | Tokeo | Mambo ya ziada |
---|---|---|---|---|
2003 | 2003 Mbio ya Dunia ya Ubingwa ya Vijana | Sherbrooke, Canada | 1 | 100 m kuruka viunzi |
5 | 200 m | |||
2003 Mbio ya Dunia ya Ubingwa | Paris, Ufaransa | mkondo wa kwanza | 4 x 100 m relay | |
2004 | 2004 Mbio ya Dunia ya Ubingwa ya Vijana | Grosseto, Uitalia | 4 | 100 m ya kuruka viunzi |
3 | 100 m | |||
5th | 4 x 100 m relay | |||
2006 | Commonwealth Games]] | Melbourne, Australia | 8 | 100 m |
2006 IAAF Mbio za Dunia | Athens, Ugiriki | 4 | 100 m kuruka viunzi | |
8 | 100 m | |||
2007 | 2007 Mbio ya Dunia ya Ubingwa | Osaka, Ujapani | semifainali | 100 m |
semifainali | 100 m ya kuruka viunzi | |||
mkondo wa kwanza | 4 x 100 m | |||
2008 | Olimpiki ya 2008 | Beijing, Uchina | 2 | 100 m ya kuruka viunzi |
2009 | 2009 Mbio ya Dunia ya Ubingwa | Berlin,Ujerumani | 5 | 100 m ya kuruka viunzi |
Muda bora(Kibinafsi)
[hariri | hariri chanzo]- 100 m - 11.14 s (2007)
- 200 m - 23.36 s (2006), 22.61 s W/S +2.1 (2009)
- 100 m ya kuruka viunzi - 12.48 s (2011)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ^ Furaha kwa warukaji viunzi huko Monaco
- ^ Hadithi ya Sally Ilihifadhiwa 24 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
- IAAF Ilihifadhiwa 21 Oktoba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Riadha nchini Australia Ilihifadhiwa 27 Juni 2009 kwenye Wayback Machine.