Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, inaangazia siku ya "ujuzi kwa vijana duniani' inayoadhimishwa kila tarehe 15 ya mwezi Julai kila mwaka, lengo ni kuwawezesha walimu, wakufunzi na vijana kutumia ujuzi wao kwa maendeleo.Leo mtayarishaji amezungumza na Tukupala Mwalyolo, msichana anayeunda ndege zisizo na rubani 'drone', pamoja na Emmanuel Cosmas Msoka, kijana mbunifu wote wakitumia teknolojia kutafuta suluhu na wako Tanzania.
Vipindi vingine
-
Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa
Msikilizaji dunia inashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miongo 6 iliyopita, ambapo mwaka 1960 idadi ilikuwa bilioni 3 lakini katika miongo miwili tu hadi mwaka 1982 ilikuwa imevuka watu bilioni 5 na November mwaka 2022 kulikuwa na watu bilioni 8 duniani.Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunajadili Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa.Tumezungumza na Walter Nguma, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania09/10/202410:03 -
Athari za utoroshaji na utakatishaji fedha barani Afrika
Tatizo la fedha haramu barani Afrika linaligharibu bara hili kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 na bilioni 80 kila mwaka, Asilimia 44 ya utajiri wa kifedha wa Afrika inadhaniwa kuwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Uwazi wa Ushuru barani Afrika ya 2023, nchi za Afrika zimeokoa dola bilioni 2 kwa mwaka kutokana na watu kuweka wazi mapato yao, ubora wa kubadilishana taarifa na uchunguzi wa nje ya nchi.Tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.02/10/202409:58 -
Fursa na changamoto ya huduma jumuishi za mifumo ya kifedha kidijitali barani Afrika
Msikilizaji kwa mujibu wa benki ya dunia, ni asilimia 49 tu ya watu wazima wanamiliki akaunti benki, takwimu za hivi karibuni zikionesha ongezeko la asilimia 55 mwaka 2021 kutoka asilimia 43 mwaka 2017, hata hivyo kiwango hiki kikiwa kidogo ukilinganisha na wastani wa kidunia wa asilimia 76. Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili tunajadili kuhusu huduma jumuishi za mifumo ya kifedha barani Afrika. Machambuzi wa masuala ya uchumi ALI MKIMO anajibu maswali kadhaa kuhusu sekta hii.18/09/202409:58 -
Afrika na usalama wa chakula
Msikilizaji juma lililopita Rwanda ilikuwa mwenyeji wa kongamano la mfumo wa chakula barani Afrika, ambapo wadau zaidi ya elfu 4 kutoka kila pembe ya mataifa ya Afrika walishiriki.Mkutano uliangazia kuhusu mifumo ya chakula, mbinu bora na teknolojia ambazo zinaweza kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula barani Afrika na wakati huohuo kutengeneza nafasi za kazi na fursa kwa wanawake.Msikilizaji wiki hii nimeshirikiana na mwanahabari wetu wa Kigali, Christopher Karenzi;11/09/202409:36 -
Ndio au hapana, mkutano kati ya Uchina na Afrika
Uchina wiki hii imekuwa mwenyeji wa mkutano kati yake na viongozi wa Afrika, kwa mujibu wa takwimu zilizoko, China ni taifa la pili duniani kufanya biashara nyingi zaidi na bara la Afrika, biashara inayokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 167 kwa mwaka. Kuangazia mkutano huu na wasiwasi ulioko kuhusu uwekezaji wa China barani Afrika, tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.04/09/202409:56