Pango (kodi)
Pango (kutoka kitenzi "kupanga") au kodi ya kupanga (kwa Kiingereza: lease au rent) ni pesa ambayo inatakiwa kulipwa kwa wakati kadiri ya mkataba kati ya mwenye nyumba au ardhi na anayepanga mali hiyo.
Kwa kawaida, kodi ya nyumba za kuishi au jengo la biashara hulipwa baada ya muda fulani ambao mwenye mali ile na anayekodi wamekubaliana. Kutolipa kodi ili huenda anayepanga akafurushwa nje au akachukuliwa hatua za kisheria kwa kutotimiza wajibu wake katika mkataba waliowekeana na mwenye nyumba. Mwenye mali kwa upande wake anafaa ahakikishe kwamba mahala pale pamefanyiwa ukarabati, anawajibika anapotakikana na mpangaji.
Sababu za kukodi au kupanga nyumba
- Huenda anayekodi hana pesa za kununua nyumba yake, kujenga au ardhi na kwa hiyo inambidi akodi.
- Huenda ukawa unahitaji nyumba au ardhi kwa muda mfupi na kwa hiyo hamna maana ya kununua mali ile ikiwa kuna anayekodisha.
- Huenda mpangaji anataka kumwachia mwenye mali kazi za kurekebisha na kukarabati mali ile na kwa hiyo anaonelea heri asinunue bali akodishe.
- Huenda anayekodi akahofia kupata hasara kwa kununua kwani mali ile inaweza kushuka bei baada ya muda fulani kwa hiyo anaonelea heri akodishe kuliko kununua.
Masuala ibuka katika kodi
Hivi leo, biashara ya kukodisha mali imekuwa kubwa sana. Kulingana na Shelter Afrique, kikundi kinachojishughulisha na mambo ya makao mema kwa Waafrika, yakadiriwa kuwa kila mwaka nyumba bilioni mbili hutengenezwa kila mwaka na kukodishwa kwa watu. Mwaka 2016, walikadiri pia kuwa asilimia arobaini (40%) ya Waafrika walikuwa wakiishi katika miji mikuu na kwa hivyo walihitaji kukodishiwa nyumba.
Kukodi ofisi za kazi
Watu wamekuwa wakikodi ofisi za kufanyia kazi kwa muda mrefu haswa katika miji ambapo wataweza kuwasiliana na wateja wao kwa urahisi. Hivi leo, kumekuwa na ofisi za kukodisha ambapo mpangaji hupata kuwa kila kitu kama samani, mtandao, simu, ukarabati wafanywa kwa ofisi yake. Anapohitajika ni kulipa tu kodi na aanze kufanya kazi kwa ile ofisi. Hatahitaji kununua fenicha, kuweka nyaya za umeme au za simu katika ofisi ile. Pia usafi wafanywa na mwenye nyumba. Pengine wapangaji ofisi hawataki kuchoka wakishinda wakipamba ofisi zao. Wataka wewe uwafanyie yote hayo.
Mtandao na kodi
Matumizi ya intaneti yamerahisisha utafutaji wa nyumba au ardhi za kukodisha. Wenye mali ya kukodisha wanaweka makala ya mali yao katika mitandao nao wapangaji wanaweza kuwasiliana na wenyewe kwa urahisi zaidi. Kulingana na utafiti uliofanywa na YouGov, asilimia sabini na sita (76%) wanaosaka mali ya kukodi wataangalia kwa mtandao kwanza kama mali wanayotafuta ipo.
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pango (kodi) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |